Programu ya Uhamisho wa Fedha: Mwongozo wa Ushuru wa Kiafrika

Tuma Pesa kwa Usalama, Haraka na pia kwa gharama nafuu kabisa!

I. Kulinganisha kwa kina watoaji huduma za uhamishaji fedha kwa pesa zinazotoka Africa 

Watu barani Afrika wameweza kuyatumia vizuri maendeleo ya usafirishaji na mawasiliano ya bara ili kuhamia mikoa na pia nchi zingine barani kwa madhumuni ya kufanya kazi.

Kufanya kazi maeneo ya mbali na nyumbani na utumaji pesa kwa familia zilizoko maeneo tofauti  kumeboresha sana hali ya maisha ya watu wengi barani Afrika. Hivi sasa, takriban watu milioni thelathini wanaishi na kufanya kazi nje ya mataifa yao asili humu Afrika.

Je! Watu hawa Huwatumia Fedha Wapendwa Wao Katika Mataifa Mingine ya Afrika?

Je! Njia zipi Zinazotumiwa, Na Je! Jukumu la Watoa Huduma za Uhamishaji Fedha Mtandaoni ni gani?

Licha ya maendeleo ya kiteknolojia ya hivi karibuni, gharama ya huhamishaji fedha kwenda Afrika imebaki kuwa ghali mno, kwa mara nyingi, ada huzidi asilimia kumi (tazama nakala hii "Ni nini kinachozuia usumbufu wa kidijitali katika uhamishaji pesa Kusini mwa Afrika?" (Januari 2019) na "Rekodi za fedha nyingi zilizotumwa Ulimwenguni” mnamo mwaka wa 2018 "(Aprili 2019), zote zimechapishwa na WorldBank).

Walakini, kutuma pesa nje ya nchi sio lazima iwe kwa gharama ya juu sana. Ukiwa na mtoa huduma sambamba wa kuhamisha pesa mkondoni, unaweza hata kuokoa pesa nyingi kwa ada ya ushuru.

Remittances to Africa 2017

Utumaji Fedha katika Kusini mwa Jangwa la Sahara 2017, iliyochapishwa kwenye DW.com

average remittance cost to Sub-Saharan Africa

Wastani wa gharama ya kutuma pesa Kusini mwa Jangwa la Sahara, iliyochapishwa kwenye Economist.com

Jinsi ambavyo Waafrika Wengi Wanavyojisimamia katika kulipa Ushuru wa Uhamishaji Fedha

Uhamishaji fedha mkondoni ni muhimu sana, haswa kwa afya ya kiuchumi ya Afrika na maskini wanaopokea pesa hizo.

Waafrika wengi wamekuwa wakitumia barua pepe za kibinafsi au kuamini kampuni za uhamishaji fedha ambazo hazina uaminifu.

Watu wangepeana madereva wa basi au lori pesa taslimu kupelekwa kwa familia, wakiwa na matumaini kwamba itapelekwa kwa mpokeaji anayefaa.

Njia nyingine ilikuwa kuchukua muda wa kupumzika kazini (kupoteza pesa wakati wa mchakato) ili kupeana fedha kwa walio mbali. Njia hizi sio salama, au za kuaminika, au za wakati unaofaa.

Tazama pia chapisho langu pana: Jinsi Mfumo wa Hawala wa Kuhamisha Fedha Unavyofanya Kazi Barani Afrika

Kuanzisha Uhamishaji wa Fedha Mkondoni na Malipo

Kuongezeka kwa upatikanaji wa mtandao barani Afrika kumeleta mambo mengi karibu na watu kama vile habari, elimu, ujumuishaji wa kijamii, na huduma za benki katika simu za rununu. Ni dhahiri kuwa hata watu wa nchi masikini zaidi barani Afrika wana simu mahiri na uafikiaji wa mtandao lakini hawana akaunti za benki (watu wasio na benki).

Hivyo basi, haishangazi kuwa uhamishaji fedha mtandaoni kupitia rununu unakuwa jibu maalum.

Uhamishaji pesa mkondoni kupitia simu za rununu, hata kwa maeneo ya mbali, ni bora, nafuu na salama. Kinachohitajika ni kwa anayepokea na anayetuma kuwa na simu za rununu na uafikiaji wa mtandao.

Benki zinaifurahia biashara ya kutuma pesa mkondoni, kwani zinaweza kutoa huduma kwa watu wa vijijini bila kuanzisha matawi zaidi. Msaada wa benki kwa utumaji pesa mkondoni una nia nyingine: wanatumaini kwamba mwishowe watu wataanza utumizi wa benki.

Soma pia nakala yangu ya Maswali kuhusu uhamishaji wa pesa nje ya nchi.

II. Aina kuu za Programu za Uhamishaji Fedha

Kimsingi kuna aina mbili kuu za programu za kuhamisha fedha. Kulingana na mahali unapoishi na lengo lako ni nini matokeo ya chaguo la programu ya kuhamisha pesa yaweza kuwa tofauti.


Uhamisho wa haraka na wa bei nafuu:


Ikiwa unataka kutuma pesa haraka na kwa bei nafuu, kwa mibofyo michache tu, basi nakushauri mwendeshaji wa kuhamisha pesa kama vile Worldremit, Xoom au Azimo. Mpokeaji wa fedha haitaji kuwa na akaunti ya benki. Pamoja na watoaji hawa wa kuhamisha pesa mkondoni unatuma au kupokea pesa zako kwa simu ya rununu au muda wa maongezi wa rununu au kwenye akaunti ya benki kwa dakika chache tu! Ni rahisi sana, kwa gharama nafuu na salama!


Ada ya chini kabisa, kiwango bora cha ubadilishaji wa sarafu, kutoka akaunti moja ya benki hadi nyingine:


Ikiwa unataka kutuma pesa zako kwa ada ya chini zaidi na upate kiwango bora cha ubadilishaji wa sarafu, basi nakushauri soko la wenzao (kwa P2P) kama vile Wise au CurrencyFair!

Kwa watoa huduma hizi za kuhamisha fedha mkondoni anayetuma na anayepokea wanahitaji kuwa na akaunti za benki. Kama faida unapata kiwango bora zaidi cha ubadilishaji wa sarafu kwa uhamishaji wako wa pesa nje ya nchi.

III. Vikundi Vinavyolengwa kwa Programu za Uhamishaji wa Fedha

Kuna tovuti nyingi nzuri sana kuhusu programu za kuhamisha fedha. Kuna tovuti kadhaa ambazo utapata programu bora ya kuhamisha pesa kwako (kwa mfano monito.com au Money Transfer Comparison).

Lakini wavuti hii kuhusu uhamishaji wa fedha mkondoni imeboreshwa haswa kwa watu walio na mwelekeo au msingi wa kiafrika:

  • Waafrika, wanaoishi na kufanya kazi nje ya Afrika (Umarekani, Uingereza, Ulaya, nk) na wanataka kutuma pesa nyumbani; k.v. wanafunzi, wafanyikazi wa kiwango cha chini, wakimbizi au wahamiaji
  • Waafrika, wanaoishi na kufanya kazi katika nchi yao ya asili, na wanatarajia kupokea fedha kutoka nje ya Afrika
  • Waafrika, wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi, katika nchi nyingine ya Kiafrika, na wanataka kutuma pesa kati ya nchi za Kiafrika.

Ushuhuda wa programu za kuhamisha fedha

Soma kile wengine wanachosema kuhusu kutumia programu za kuhamisha pesa kutuma au kupokea fedha:

Bukunmi Adetayo for WorldRemit

Ni haraka sana na inapatikana kwa urahisi. Namaanisha huyu ni ‘flash man’. Inanisaidia kuongeza matumizi yangu ya huduma za OPay. Nadhani kuna faida ninazofurahiya kama mtumizi wa huduma za OPay.

Bukunmi Adetayo muuzaji wa kidijitili

Nicholas Kariuki money transfer app

Lazima nithamini juhudi za Jens katika kuifanya Afrika ielewe teknolojia. Mimi binafsi nina uzoefu mzuri tangu nilipojifunza kuhusu Worldremit kutoka kwa nakala za Jens. Ninashukrani kwani ninapokea malipo mara moja na hakuna malipo ya ubadilishaji wa sarafu kwa upande wangu. Asante Jens.

Nicholas kariuki Mfanyikazi huru - Kenya

Charles testimonial for money transfer apps

Nakala yako ilikuwa hakiki. Watu wengi ambao sio Waafrika ambao hawajawahi kuingia katika Bara hili wana maoni ya mapema juu ya Afrika. Kama ilivyoelezwa katika nakala yako, Afrika sio Nchi. Tuna akili nzuri na wavumbuzi kwa idadi kubwa Afrika. Suluhisho la changamoto za Afrika lazima lije kutoka kwa Waafrika.

Charles Moseti Msaidizi wa Utafiti katika Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa

Christine Rombe money transfer app

Ndio, nimetumia programu za kuhamisha fedha, moja wapo ikiwa Payoneer. Programu hii imekuwa ya kushangaza sana kwangu kwani inaruhusu miamala laini (unaweza kuitumia kutuma au kupokea hela katika nchi tofauti ulimwenguni) pia inatoa sarafu zaidi ya mia moja. Kama Mfanyikazi huru, nimeichagua zaidi ya programu zingine mara kadha wa kadha kwani inatoa viwango vya ushindani vya ukarimu.

Christine Rombe Kiongozi Mwandishi wa Maudhui / Muumbaji katika Swipe Solutions Health / Fitness Professional

Frank Mugambage money transfer app review

Hakika ninafurahi kutumia Worldremit kutuma pesa nje ya Marekani. Inafanya iwe rahisi na haraka kutuma pesa popote ulimwenguni.

Frank Mugambage – Mwanafunzi

IV. Sababu nzuri za Kutumia Programu za Uhamishaji wa Fedha

Urahisi


Programu za kuhamisha pesa ni muhimu sana na rahisi kutumia. Ukweli ni kuwa unaweza kutumia programu za pesa popote, wakati wowote, hivyo basi ni muhimu sana na zinafaa.


Huduma za bei nafuu


Hapo awali wakati njia pekee ya kukamilisha uhamisho ilikuwa kupitia mawasiliano ya kibinadamu, huduma hiyo ilikuwa ghali mno.


Usalama


Watu wanaochukua hatua haraka ndio wanaotumia programu za kuhamisha. Watu kama hao wanafurahia ulinzi wa hali ya juu wa data zao zote za kibinafsi au za kifedha.


Malipo ya haraka


Kutumia programu ya kuhamisha hela ni haraka. Sasa, unaweza kuhamisha pesa kwa familia yako au marafiki kwa upesi.


Tazama pia chapisho langu kwenye Quora linalohusu sababu za juu za kutumia programu ya kuhamisha pesa: Je! Ni bora kuhamisha pesa nje ya nchi ukitumia Uhamishaji wa Benki (SWIFT) au Huduma za Uhamisho wa Fedha, kama Western Union au Money Gram?

V. Watoaji Huduma Bora za Uhamishaji wa Fedha Mkondoni Wanaopatikana katika Nchi za Kiafrika

Programu za kuhamisha hela ni sehemu muhimu, unahitaji moja kuweza kuhamisha pesa zako kwa urahisi na salama.

Ikiwa uko ndani ya nchi ya Kiafrika, programu ya kuhamisha pesa mkondoni ni muhimu. Kwa kuongeza, kuna tofauti kwa chaguo la mtoaji wa programu ya kuhamisha pesa ikiwa unataka

  • tuma pesa kutoka nchi ya Kiafrika (kama vile Afrika Kusini kwenda Umarekani au Uingereza)
  • tuma pesa kwa nchi ya Kiafrika (kwa mfano Umarekani kwenda Nigeria au Kenya)
  • tuma pesa kati ya nchi za Kiafrika (kwa mfano Tanzania kwenda Ghana)

Unahitaji kuzingatia:

  • ada ya jumla
  • huduma kwa wateja
  • utulivu wa programu
  • msaada wa nchi
  • viwango vya ubadilishaji

Utafutapo programu dhabiti ya kuhamisha pesa. Sio rahisi kupata moja lakini tunakusudia kukusaidia katika utafutaji wako kwa kutoa suluhisho tano maalum za uhamishaji wa hela ndani ya nchi za Kiafrika.

Programu hizi zote zinasaidia nchi hizi za Kusini, Mashariki na Magharibi mwa Afrika kwa huduma ya hali ya juu.

Kesi ya nchi Nigeria: Soma jibu langu katika Quora: Je! Ni njia gani bora na salama ya kutuma fedha Nigeria au nchi zingine za Kiafrika kutoka Marekani au Uingereza?

VI. Mafunzo ya Nchi juu ya Uhamisho wa Fedha

Ili kukupa ushauri kamili naandaa orodha ya ripoti za uhamishaji wa pesa zinazoonyesha hali halisi na changamoto kwa nchi tofauti za Kiafrika.

Hadi sasa nakala zifuatazo zimechapishwa:

VII. Mapendekezo Yangu ya Uhamishaji wa Fedha

WorldRemit      


WorldRemit ni suluhisho la malipo linalojulikana kwa viwango vyake vya ushindani, njia anuwai za malipo, orodha ndefu ya nchi zinazoungwa mkono, njia za kuhamisha, nyakati za haraka za kubadilisha na msaada thabiti wa wateja kwa njia ya mazungumzo ya moja kwa moja na chaguzi za simu. WorldRemit kwa sasa inasaidia nchi takriban mia moja na kumi, chache kati ya hizo zikiwa kutoka Afrika na Mashariki ya Kati. Jambo la kupendeza kuhusu WorldRemit ni kwamba wanapeana kuponi ambazo zinaweza kuwa na faida kwa wahamishaji wapya waliowasili, kuponi hizi zinaweza kuruhusu uhamisho wako wa kwanza kuwa bure kabisa au ada iliyopunguzwa kwa mabadilishano yatakayofuata.

Viwango vya ubadilishaji vya WorldRemit ni kati ya busara Zaidi na huduma yao kwa wateja ni ya kipekee. Kampuni hii inapendekezwa sana na wateja kwa matoleo kama haya, kiwango chake cha juu cha uaminifu kwenye TrustPilot kinajieleza. WorldRemit ni chaguo bora la programu za kuhamisha hela.

Mwongozo mpana kuhusu Worldremit: bonyeza kiungo hiki!


Azimo


Azimo ni chaguo la tatu kwenye orodha yetu ya programu za kuhamisha fedha, kampuni ilianzishwa mnamo mwaka wa 2012 nchini Uingereza. Jukwaa hili bado ni mpya na halijulikani kwenye soko lakini kwa ukuaji wa muda na kuendelea, wanaweza kuwa maarufu. Wana sarafu 198 zinazopatikana kwa biashara na ubadilishaji, kiwango cha chini cha uhamishaji ni Pauni moja. Azimo inapatikana kwenye vivinjari vingi, kwa sasa hakuna programu ya vifaa vya rununu na kompyuta. Kutumia Azimo kwenye vifaa hivi ni kwa kupitia wavuti rasmi, usiwe na wasiwasi juu ya utulivu na uaminifu kwa sababu wavuti ni uzoefu mzuri wakati mwingi, tofauti na programu zingine za kuhamisha pesa ambazo zinategemea tovuti zao tu. Azimo inasimamiwa na kupewa leseni na Mamlaka ya Maadili ya Fedha nchini Uingereza, hivyo basi usalama na uhalali umehakikishwa.

Kinachotofautisha Azimo na programu zingine ni msaada wake kamili kwa watu wengi wa nchi za Kiafrika. Inayo misaada kwa nchi hamsini za Kiafrika kama vili Algeria, Chad, Nigeria na zinginezo ambazo zinaweza kupatikana hapa.

Wakati msaada wa Azimo kwa Mashariki ya Kati hauwezi kufikia viwango hivi, inaweza kutumika kwa nchi nyingi katika eneo hilo.

Mwongozo mpana kuhusu Azimo: bonyeza kiungo hiki!


CurrencyFair


Mchakato wetu wa malipo unaofuata kwenye ukaguzi leo ni CurrencyFair, kampuni iliyoanzishwa mnamo mwaka wa 2010, sarafu 18 ziko kwa biashara na ubadilishaji. CurrencyFair inasisitiza kiwango cha chini cha uhamisho, kwa hivyo unaweza kuhamisha kiwango chochote unachotaka.

Wanazo ofisi nchini Uingereza, Australia na Ireland. Udhibiti wa kuridhisha na leseni ni pamoja na zile kutoka Benki Kuu ya Ireland na Tume ya Usalama na Uwekezaji ya Australia, hizi hufanya CurrencyFair kuwa programu halali na salama ya kuhamisha hela ya kutumia.

CurrencyFair sasa inadumisha kiwango cha ajabu cha asilimia tisini na mbili kwenye TrustPilot, makubaliano ni kwamba ni suluhisho kamili la uhamishaji wa fedha. CurrencyFair inapatikana katika nchi tofauti, ikiwemo zile za Mashariki ya Kati na Afrika

Mwongozo wa kina kuhusu CurrencyFair: bonyeza kiungo hiki!


Wise


Wise ni ya pili katika orodha yetu ya programu za kuhamisha fedha, ilianzishwa mnamo mwaka wa 2011. Kwa sasa, Wise inaunga mkono sarafu 38, ingawaje huwezi linganisha na Payoneer inayohusisha sarafu mia moja hamsini, bado ni pendekezo muhimu sana kwa wahamiaji wa Mashariki ya Kati na Afrika kwani kuna mengi ya kujivunia kwa mikoa hii miwili. Ili kufikia Wise, unaweza kutumia wavuti mkondoni au programu kutoka kwa simu yako ya rununu. Pamoja na ofisi huko Marekani, Uingereza, Australia, Estonia, Hungary, Japan na Ukraine. Wise ina msaada mzuri sana kote ulimwenguni. Kwa sasa ni suluhu maarufu la malipo kati ya wateja kama inavyodhihirishwa na umaarufu wa asilimia 95 kwenye tovuti ya hakiki TrustPilot.

Wise ina msaada mkubwa sana kwa sarafu ya India inayoitwa Wise India. Pia ina kiwango cha juu cha uwazi kwa bei zake, kiwango cha juu cha biashara, usalama na uaminifu, orodha ya tuzo za majukwaa ya malipo, uvumbuzi, kuridhika kwa wateja na msaada kwa kila aina ya uhamisho. Mbali na India, Wise inapeana ubadilishaji kwenda na kutoka sarafu maarufu ya Afrika Kusini ya ZAR na viwango bora na huduma nzuri kwa wateja. Wakazi wengi Afrika Kusini wamehakikisha huduma wanazopewa na Wise. Walakini kuna mambo mawili muhimu ambayo unapaswa kutambua, kwanza ni malipo ya Wise; Jumuiya ya Mawasiliano ya Fedha Duniani ambayo inaamuru kwamba uhamisho lazima upitie rundo la benki kabla ya kufikia mwisho wake (akaunti yako ya benki), uhamisho unaweza kupata ada kwa sababu ya benki anuwai ambazo hupita. Ujumbe wa pili ni kwamba kwa sasa hivi, Wise haina kumbukumbu za uhamishaji kutoka Afrika Kusini, hivyo basi unahitaji kujaza fomu ya mwongozo kwenye wavuti rasmi ili kusaindika.

Kwa jumla, Wise ni suluhu maarufu kati ya programu nyingi za kuhamisha fedha. Inawasaidia wahamiaji wa Kiafrika / Mashariki ya Kati, wakimbizi na jumla ya wahamiaji kwa nchi nyingi ndani ya maeneo hayo.

Mwongozo mpana kuhusu Wise: bonyeza kiungo hiki!


Payoneer


Mwishowe, kuna Payoneer, jukwaa maarufu la malipo lililoanzishwa mwaka wa 2005. Payoneer hutoa huduma na faida nyingi. Kwa sasa inatoa uteuzi wa kina wa sarafu mia moja hamsini pamoja na zile zinazoungwa mkono katika Mashariki ya Kati na nchi za Afrika. Programu za malipo zinapendekezwa kwa wafanyibiashara huru wa mitandaoni, wanabiashara wengine. Washirika wakuu wa payoneer ni pamoja na kampuni kubwa za mtandao kama vile Google, Amazon, UpWork na Getty Images. Wanazo ofisi katika nchi kadhaa kama vile Marekani (San Fransisco na North Carolina), Israeli (Tel Aviv), Uingereza (London), Uhispania, Uchina (Beijing) Japani, Ufilipino na India. Kampuni hiyo inausawa na kanuni za soko, wana leseni kutoka kwa Tume ya Huduma za Fedha, Idara ya Forodha na Ushuru na Money Transmitter. Payoneer ni programu ya kimataifa ya uhamishaji fedha yenye umaarufu, ni jukwaa pana na lenye uwezo mwingi.

Payoneer ina kiwango cha ushindani kwa huduma kama ada ya kutuma fedha, malipo maridadi ya asilimia mbili ya fedha za kigeni, gharama ya chini ya dola 29.99 kwa Payoneer kadi kuu na ada ya kawaida ya kadi kuu. Programu nyingi za kuhamisha hela hazitoi huduma kama hizo. Hii inaweza kuwa ya thamani kubwa kwa mhamiaji mpya kwenda nchini kutoka Afrika Kusini au nchi ya Mashariki ya Kati kama Israeli. Ukiwa katika nchi mpya inaweza kuwa ngumu kutuma hela lakini Payoneer hufanya iwe rahisi kwa msaada wao mkubwa, matoleo anuwai na ada nafuu. Kuzingatia washirika wake wakuu, unaweza kuwa na hakika kuwa Payoneer ni jukwaa salama kabisa. Google na Amazon wangesita kufanya kazi nao vinginevyo iwapo sio waaminifu.

Mwongozo mpana kuhusu Payoneer: bonyeza kiungo hiki!

Mwishowe

Kila soko la uhamishaji fedha au soko la ushirikiano (P2P) lililojadiliwa hapa lina uwezo wa kukidhi mahitaji yako ya kifedha, haswa ikiwa yanahusu sarafu za Kiafrika.

Inapendekezwa sana kwamba ukague zaidi tovuti zilizotajwa ili kujua ipi inayokufaa. Programu za kuhamisha fedha zinaweza kuwa jambo ngumu kubaini lakini ni matumaini yetu kwamba kupitia mwongozo wetu, unaweza kupata moja ambayo itatimiza mahitaji yako.