Malipo ya Utumaji Fedha kote Afrika
Shughuli za utumaji hela kote Afrika zinaendelea kuongezeka kwa kasi mno.
Pesa za kidijitali zinahamishwa kila wakati kati ya nchi za Bara la Afrika. Sehemu kubwa ya uhamisho unaoenda Afrika ni kutoka nchi kama vile Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Marekani.
Waafrika wengi wamehamia ng’ambo kutafuta ajira, kutorokea vita au kuendeleza masomo.
Lakini kila mtu anahitaji njia za kuaminika na salama za kuhamisha hela mkondoni anapotuma pesa nyumbani.
Je! Ulipata shida yeyote kupata mtoa huduma za kuhamisha fedha mkondoni wakati ulihamia nje ya nchi?

Ada za Juu za Benki
Kutumia mifumo ya jadi ya uhamisho kwa kutumia benki kutuma pesa kwa nchi za Kiafrika huleta ada kubwa mno. Inaweza kuwa juu mara kumi zaidi ya wale wanaohusika katika uhamishaji wa pesa za dijitali.
Akaunti ya benki inahitajika
Waafrika wengi wanaoishi ng’ambo kawaida wanatarajia kuanza kuhamisha fedha kupitia benki. Walakini, kuna wakati ambapo haiwezekani kufungua akaunti.
Muda mrefu wa Uhamisho
Iwapo unafanya kazi ng’ambo ili kupata pesa Zaidi za kusaidia familia yako barani Afrika basi unahitaji wapate hela hizo kwa haraka iwezekanavyo. Shughuli za kuhamisha pesa kupitia njia za jadi za benki ni mbovu mno. Zinaweza kuchukua hadi siku tano za kazi kufanikisha ambazo kwa kweli zitachelewa kwa wiki.
Utafiti wa haraka: Je! Mbona unahitaji uhamishaji wa pesa mkondoni? Je! Nia yako ni ipi na lengo lako ni lipi?
Tumia tu dakika mbili za wakati wako na unisaidie kwa utafiti huu wa haraka.
Malipo ya papo hapo ya Uhamisho wa Pesa Mkondoni
Kutuma pesa na mfumo wa uhamishaji wa hela mkondoni ni haraka mno.
Fedha zako zinalindwa kupitia usimbuaji fiche wa usalama wa SSL na zinaweza kupatikana kwa urahisi na jamaa zako kupitia simu mahiri au kutoka kwa hatua ya malipo iliyoidhinishwa. Je! Wewe au familia yako mmefaidika na hela zilizotumwa kupitia mmoja wa watoa huduma za uhamishaji fedha mkondoni waliotajwa kwenye wavuti hii?
Pochi Mbadala za Pesa za Dijitali katika Uhamisho wa Pesa Mkondoni
Baadhi ya watoa huduma maarufu wa kuhamisha fedha mkondoni kama vile PayPal, hawapo Afrika au wana uwepo mdogo. Kufanya utaftaji mkondoni kutaonyesha orodha za mifumo ya benki ya dijitali ya uhamishaji fedha, lakini sio zote ambazo ni za kuaminika. Nijulishe ikiwa umekuwa na bahati mbaya na kutapeliwa na mifumo isiyofaa.
Utumizi wa Mfumo wa Uhamishaji Hela Mkondoni wa Hawala
Mfumo wa Hawala unafahamika vyema nchi nyingi za Kiafrika ingawaje hauhakikishi usalama wa shughuli zako au maelezo yako ya kibinafsi. Inajulikana kwa usiri na haijasimamiwa na taasisi yeyote ilio na mamlaka rasmi. Programu za kuaminika za uhamishaji hela zinazorejelewa kwenye wavuti hii zinasimamiwa rasmi na kupewa leseni ya kukupa amani dhabiti.
Tazama chapisho langu pana: Jinsi Mfumo wa Hawala wa Kuhamisha Fedha Unavyofanya Kazi Barani Afrika
Kwanini nimehamasishwa kuunda Wavuti ya Programu za Uhamishaji Fedha
Nimefanya kazi na vijana wengi kutoka Afrika wanaotafuta riziki yao ng’ambo na nikavutiwa na bidii yao na dhamira ya kufanikiwa.
Wengi wanatamani sana kusaidia familia zao barani Afrika kwa kuchangia katika masomo ya ndugu zao au kuwatunza jamaa zao wakongwe.
Kwa wengine ni matarajio kuwa wataboresha nchi zao katika miradi anuwai ya ustawi wa jamii.
Ujumbe wangu unasaidia kuchagua watoa huduma waaminifu wa Uhamishaji wa Fedha Mkondoni
Ninazifahamu shida wanazokumbana nazo vijana wengi wa Kiafrika katika mifumo ya jadi ya benki.
Kuwa katika rehema ya huduma za uhamishaji wa pesa zisizofaa ni msimamo ambao singependa.
Dhamira yangu ni kutoa habari kwa kina iwezekanavyo kukusaidia kupata moja ya programu za kuaminika za kuhamisha fedha.
Uzoefu wangu binafsi wa Uhamishaji Fedha Mkondoni
Miaka kadhaa iliyopita nilihitaji kuhamisha pesa kwenda Kiafrika kupitia benki yangu.
Mimi ningeweza kumudu ada lakini kijana wa Kiafrika aliye mbele yangu kwenye foleni alisikitika kugundua kwamba pesa nyingi alizopata kwa bidii zilipaswa kutolewa ada kubwa kwa njia hii.
Kama mshauri mwenye uzoefu wa fintech (teknolojia ya kifedha) nilifahamu mifumo mbadala ya uhamishaji hela kidijitali ndipo nkaamua kugawa maarifa yangu.
Tovuti yenye taarifa inayotolewa kwa Uhamisho wa Fedha Mkondoni
Niliunda tovuti yangu ya fintech mwaka wa elfu mbili kumi na tano na nilielezea kwa undani watoa huduma maarufu wa kuhamisha hela mkondoni ambao wana utaalam katika kuhamisha pesa kwenda Afrika.
Kilichonishangaza ni idadi kubwa ya Waafrika waliowasiliana nami kuhusu jinsi ushauri wangu umewasaidia kuchagua kwa busara.
Maoni yao yalinifanya nitambue mchango mzuri kwa jamii.
Kwa matarajio yeyote ya biashara, analeta kwenye meza utajiri wa ufahamu, utoaji mzuri na wa wakati unaofaa, na kujitolea kwa kiwango cha juu katika kufikia malengo yaliyowekwa.
Roy Tanga Mwanablogi Huru katika Chama cha Wanablogi wa Kenya
Tovuti za Jens zinaonyesha kuwa ana nia pana, na anapendelea teknolojia mpya na zinazoibuka. Yeye ni mfano bora wa mtu anayeunganisha Ulimwengu!
Catherine Mong'ina CISA
Nakala yako ilikuwa hakiki. Watu wengi wasio Waafrika ambao hawajawahi kuingia katika Bara hili nzuri wana maoni ya mapema juu ya Afrika. Kama ilivyoelezwa katika nakala yako, Afrika sio Nchi. Tuna akili nzuri na wavumbuzi kwa idadi kubwa Afrika. Suluhisho la changamoto za Afrika lazima lije kutoka kwa Waafrika.
Charles Moseti Msaidizi wa Utafiti katika Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa
Jens ni mtu mbunifu sana, na shauku yake ya kuboresha hali barani Afrika ni dhahiri sana. Hamu yake kushiriki kwenye habari za busara ni ya kupendeza na ninaamini ana vitu vingi zaidi.
Nana Boatemaa Amoah the Scribe-Gh
Ninapendezwa na kile Jens anachokifanya kwa Waafrika na ningependa kuchangia. Imeelekezwa kwa undani sana na imetoa matokeo mazuri kwa kampuni ...
Felicien Ihirwe Mhandisi wa Programu
Kwa kweli, Jens ni wa ajabu, mtu mzuri na mwenye shauku ambaye lazima utamshanga kwa kazi zake nzuri sana katika ulimwengu wote haswa wanafunzi wa Afrika. Anataka watu kama mimi pia kufikia malengo yangu yanayokwamisha wengi kupata elimu ya juu zaidi. Asante
Edward Atowackah BLAY
Je! Una uzoefu na programu za kuhamisha pesa ambao ungependa kugawa? Nakualika uongeze ushuhuda!
Ushauri kuhusu Huduma za Uhamisho wa Hela Mkondoni
Wavuti yangu inatoa ushauri hakiki wa uendelezaji kwa waendeshaji wanaoheshimika, walioidhinishwa kikamilifu wa uhamishaji fedha (MTO).
Kuna uwezekano tayari unayafahamu majina kadhaa kama Wise, CurrencyFair, Xoom, Azimo na WorldRemit.
Iwapo una hamu ya kujua jinsi huduma zinazojumuishwa, jifunze zaidi kwa kufuata viungo vinavyofaa.
Yalioangaziwa kwenye tovuti maarufu
Nakala zangu zimechapishwa kwenye wavuti nyingi, hapa kuna zingine maarufu:
Kunihusu
Jina langu ni Jens Ischebeck. Niko nchini Ujerumani na nina uzoefu wa miaka mingi katika huduma za kuhamisha hela mkondoni.
Halaiki wa Kiafrika walinivutia na wema na uwazi wao wa teknolojia mpya.
Athari ya Kenya kwa matumizi ya simu za rununu kufanikisha malipo (MPesa) ilikuwa mfano mzuri wa fursa kubwa zilizoundwa na idadi hii ya vijana wa Kiafrika.
Tangu mwaka wa elfu mbili kumi na sita ninaendesha wavuti ya programu za kuhamisha hela kama aina ya mwongozo wa uhamishaji / usafirishaji mkondoni kwenda, kutoka na ndani ya nchi za Kiafrika.

Wasiliana nami
Kwenye Facebook Messenger: Wacha tuzungumze pamoja!
Kwenye WhatsApp: Nitumie ujumbe WhatsApp!
Kupitia barua pepe: barua pepe kwa Jens